$datum='2009-03-11'

Blogga i tungor

($skribent='Tobias Rydén', $tid='08:04') {

'.........Fuateni upendo na kutaka sana karama za Roho, hasa karama ya unabii. Kwa maana anayesema kwa lugha, hasemi na watu bali anasema na Mungu. Hakuna mtu anayem welewa, kwani anasema siri katika Roho. Lakini anayetamka neno la Mungu anasema na watu akiwasaidia kupata nguvu, na kuwatia moyo na kuwafariji. Anayesema katika lugha anajijenga mwenyewe, lakini anayetoa neno la Mungu analijenga kanisa. Ningependa ninyi nyote mseme kwa lugha ngeni, lakini ningependa zaidi nyote muweze kutoa una bii kwa kuhubiri neno la Mungu. Kwa kuwa anayehubiri neno la Mungu ni mkuu kuliko anayesema kwa lugha, isipokuwa kama kuna mtu wa kutafsiri, ili kanisa zima liweze kusaidika. Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha ngeni, nitapata faida gani kama sikuwaletea mafunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho? Hata vyombo vya muziki visivyo na uhai kama vile filimbi au kinubi, visipotumiwa kwa mpangilio wa sauti, ni nani atakayeweza kufahamu ni wimbo gani unaimbwa? Na kama baragumu ikitoa sauti isiyoeleweka, ni nani atakayej iandaa kwenda vitani? Hali kadhalika na ninyi. Kama mkisema kwa lugha isiyoeleweka, watu watafahamuje mnachosema? Kwa maana mta kuwa mnasema hewani. Bila shaka ziko lugha nyingi ulimwenguni, na hakuna lugha isiyo na maana. Lakini ikiwa sielewi maana ya lugha inayotu mika nitakuwa mgeni kwa yule anayezungumza, naye atakuwa mgeni kwangu. Hali kadhalika na ninyi. Kwa kuwa mna hamu ya kuwa na karama za Roho, wekeni bidii katika karama zinazolijenga kanisa. Kwa hiyo anayesema kwa lugha aombe kupewa kipawa cha kutafsiri lugha. Kwa maana nikiomba kwa lugha roho yangu inaomba, lakini akili yangu haishiriki. Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho na nitaomba kwa akili yangu pia. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia. Vinginevyo, kama mkim sifu Mungu katika roho, mtu mwingine ambaye anashiriki katika mkutano wenu na ambaye haelewi atawezaje kusema, `Amina Mnaweza kuwa mnatoa shukrani kweli, lakini huyo mtu mwingine hajengeki. Namshukuru Mungu kwamba mimi ninasema kwa lugha kuliko ninyi nyote. Lakini hata hivyo, nikiwa kanisani, ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno elfu kumi kwa lugha. Ndugu zangu, msiwe kama watoto wadogo katika kufikiri kwenu. Kuhusu uovu muwe kama watoto wachanga, lakini katika kufi kiri, muwe watu wazima. Imeandikwa katika sheria, Kwa njia ya watu wenye lugha ngeni na kupitia midomo ya wageni, nitazun gumza na hawa watu, lakini hata hivyo hawatanisikiliza, asema Bwana..........'

}

0 kommentarer:

Skicka en kommentar